Senator wa New York
Malcom Smith
amtaka lil Wayne atubu.
Wyne.
Maojiano ya mtumzima Wayne sikuchache zilizo pita kupitia Mtv jamaa alisikika akisanuka kuwa anaichukia New York.
Yawezekana Wayne hakuwa na maana mbaya bali ni vile hakueleweka kama alivyomaanisha. Yawezekana alichojaribu kumaanisha ni kwamba anauchukia mji huo kwakuwa kila mara anapotimba pande zile huwa anakutwa na mikasa mbali mbali na vyombo vya sheria na kujikuta kituo cha polisi mara kwa mara.
Sasa Senator wa mji huo Malcom Smith amepiga stori na vyombo vya habari na kufunguka kwamba jamaa anatakiwa aombe msamaha kwa kauli yake hiyo ya kusema anauchukia mji wa New York endapo haita kuwa hivyo basi biashara yoyote ile inayo muhusu Lil Wyne haito fanyika katika mji huo na watazuia mauzo yote ya kazi zake pamoja na wasanii wake.
Birdman nae alikuwa anafanya interview na ''FUSE'' na pia akaulizwa juu ya kauli alizotoa Lil Wayne za kuichukia New York. Unataka kujua alisema nini? Inawezekana New Yorkers hawatapenda alichokisema yeye pia ila kwao wao ni, ''LIKE FATHER LIKE SON ANACHOSEMA WAYNE NI SHERIA


No comments:
Post a Comment