Jamani Sihusiki na kifo cha KANUMBA.

Stori zilizo enea mitaani nikwamba Ray anahusika na kifo cha muigizaji wa runinga Stevin Kanumba, Alicho kisema baada ya kuamua kufunguka kutokana na kuhusishwa na tukio hilo.
sio kweli kwa sababu Kanumba ni mdogo wangu wa karibu sana tumetoka mbali sana kimaisha mimi na yeye, nimekua na mazoea ya kuona vitu kila siku vinaandikwa ambapo juzi nilipigiwa simu na kuambiwa nitazame kwenye blog ya U Turn ambayo anaimiliki huyu dada ambae simfahamu anaitwa Mange Kimambi” “Alikua ameandika kwamba amepata taarifa kutoka kwa polisi mmoja wa Osterbay kwamba Ray ndio aliepiga simu kwa Lulu siku ya kifo cha Kanumba kwa hiyo Lulu ametumika kufanya mauaji bila kujijua, na pia kukawa kuna swali kwamba kwa nini Ray alikua wa kwanza kufika kwa marehemu Kanumba, Mungu ndie anaejua. kwa hiyo anataka kuwadhihirishia watanzania kwamba Ray ndio anahusika na hicho kifo, baada ya hilo nimeshirikiana na polisi na kushitaki na kufungua kesi ambapo hivi sasa ninapozungumza yupo polisi Osterbay akihojiwa kwa sababu ameandika kitu ambacho bado kipo ndani ya uchunguzi.
No comments:
Post a Comment