KESI YA ELIZABETH
MICHAEL LULU
YASIKILIZWA
LEO
Mbele
ya hakimu mkazi wa mahakama ya Kisutu jijini
Dar es salaam. Bi
Augustina
Mmbando mapema leo msanii wa filamu
Tanzania ambaye anahusishwa na kifo
cha msanii mwenzake pia wa filamu Steven Kanumba
amesimama kizimbani
akikabiliwa na shtaka hilo
na kesi hiyo.Utata uliibuka wakati Mawakili
wanao
mtete Lulu Keneth Fungamtama, Fulgence Massawe,
Peter Kibatala na
Jackline De Meero,
kwamba kutokana na umri mdogo wa mtuhumiwa
wanaiomba
Mahakama itoe udhuru kwa mtuhumiwa Elizabeth
kushitakiwa
katika Mahakama ya watoto kwa kuwa ana
umri chini ya miaka 18 pia kesi
yake iwe INCAMERA
ombi ambalo lilitupiliwa mbali na mahakama hiyo
kwa
kutumia kifungu cha sheria namba 196 kuwa Mahakama hiyo
haina mamlaka ya kusikiliza kesi za jinai hivyo ameahirisha kesi hiyo
hadi Mei 21 mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.
Hivyo Lulu amerudishwa Segerea hadi kesi yake itakapotajwa tena.

No comments:
Post a Comment